Compressor
Compressor ni plugin inayodhibiti tofauti ya sauti kati ya sehemu tulivu (quiet) na sehemu zenye kelele kubwa (loud) Inafanya hivyo kwa kupunguza volume ya sehemu kubwa sana halafu mara nyingi inaongeza kiasi cha volume ya jumla (make-up gain)
Matokeo yake: sauti inakaa sawa zaidi imara na thabiti bila kuruka sana kwenye volume
Vipimo muhimu kwenye compressor
Threshold kiwango cha dB ambacho compressor inaanza kufanya kazi
Ratio kiwango cha compression (mf 2:1, 4:1, 10:1)
Attack muda compressor inachukua kabla ya kushika peak baada ya sauti kuvuka threshold
Release muda compressor inachukua kuachia baada ya signal kushuka chini ya threshold
Make-up Gain kuongeza volume baada ya compression ili kurudisha nguvu iliyopungua
Kwanza ikumbukwe kuwa compressor zipo nyingi na tofauti tofauti nakusudia kitabia na katika utengenezaji wake wa tone ya kitu
hususa kwenye vocals.
Leo tutazungumzia compressor ya kawaida ambayo watu wengi wanaitumia — compressor inayotengenezwa na Waves bundle
RCompressor
Compressor hii iko na sehemu Kuu 5:
- Threshold
- Ratio
- Attack
- Release
- Gain
Threshold
Hapa ndipo compressor huanza kufanya kazi yake, na itafanya kazi kulingana na kile kiwango ambacho wewe umeruhusu ianze kufanya kazi
katika kiwango fulani cha dynamics au baada ya kiwango fulani cha vocals kufikiwa
Ukitazama hapo tumeweka
Threshold ya -14.9 Hivyo Sauti itakayo pita hapo ndio Itakayo fanyiwa
Compression
Ratio
Sehemu ya Ratio inasaidia kupunguza tofauti kubwa za volume Compressor inachukua thamani ulioiweka wewe kwenye threshold Kisha inatoa sauti inayo ingia input kisha inapata kiasi kilichozidi Juu ya threshold na kukigawa kwa ratio uliyoweka Kumbuka katika sehemu ya threshold ndipo kuna input yaani input nikile kiwango cha sauti au peak original inayoingia katika Compressor sehemu hii utaiona katika sehemu ya threshold Tazama hapa chini katika picha
Ukitazama katika picha ya chini inaonyesha
input inayoingia kwenye Compressor kwa sasa ni
-8.2
je? Compressor inafanyaje kazi kwa sasa?
Ukweli ni kwamba Compressor inafanya Mahesabu Yenyewe Kupitia Vigezo ulivyo weka wewe katika
threshold na
Ration Mfano wa vigezo katika Picha zetu
Threshold ni
14.9 ratio ni
3.01 input ni Automatic hivyo iyafanyiwa Compression Kulinga na vile inapanda na kushuka sisi Tuchukulie
Input yetu ni
-8.2Kama inavyo onekana kwenye picha Hapo juu
Jinsi inafanya kazi
Attack
Attack inakagua muda compressor inachukua kuanza kukandamiza sauti baada ya vocal kuvuka threshold.
- Fast attack: Hufaa kudhibiti consonanti kali kama P au T
- Slow attack: Huruhusu mwanzo wa vocal (transients) kubaki natural
Release
Release inakagua muda compressor inachukua kuacha kukandamiza baada ya vocal kurudi chini ya threshold.
- Fast release: Hufaa kwa vocal zenye maneno mafupi na rhythm yenye haraka
- Slow release: Hufanya vocal ibaki smooth na isikike imara bila “pumping”
Gain
Baada ya compression, kiasi cha nguvu cha vocal kinaweza kuonekana kidogo Sehemu ya Gain (make-up gain) inarudisha volume ya vocal ili ibaki audible na imara ndani ya mix